Matthew 26:31-35

31 aKisha Isa akawaambia, “Usiku huu, ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “ ‘Nitampiga mchungaji,
nao kondoo wa hilo kundi watatawanyika.’

32 bLakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

33Petro akajibu, “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.”

34 cIsa akamjibu, “Amin, nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”

35 dLakini Petro akasisitiza, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wanafunzi wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Isa Anaomba Gethsemane

(Marko 14:32-42; Luka 22:39-46)

Copyright information for SwhKC